kwanza
mwanafunzi anatakiwa ajitambue kwamba yeye ni nani, na wajibu wake ninini kama mwanafunzi na kuachana kabisa na mambo ya kufuata mikumbo isiyo faa.Ninapozungumzia kujitambua ninamaanisha kuwa uelewa wa mtu binafsi katika kungamua yeye ni nani,anapaswa kufanya nini, kwa sababu ipi.lini na katka muktadha upi.Elimu hii ya kujitambua ni adimu mno! Kwani hujikita ndani ya nafsi ya mtu na kumfanya kuonekana mwenye busara na hekima katika uongeaji ,kimaamuzi na kimatendo.
faida kuu za kujitambua
-Kila akifanyacho mwanafunzi anayejitambua hulenga kuchochea na kuleta maendeleo katika masomo yakeØ Kuwa na msimamo dhabiti katika masomo bila kuyumbishwa na mtu yoyote.
Ø Kufikia malengo chanya.
Ø Huwa kioo cha jamii (unakuwa barua isomwayo na kila mtu katika jamii).
Ø Kutenda matendo mema ikiwemo nidhamu uwapo ndani ya shule,na katika jamii inayokuzunguka
Ø Kuwa mtu usiyekuwa na makuu, pia kuwa na matumizi mazuri ya rasliamali.mfano raslimali watu,,pesa n.k
Ø uwe ni mtu wa watu.
Ø uwe mbunifu (Creative) husoma nyakati.
Ø Toa suruhu katika jambo linalokusibu na sio kulalamika au kuanza kulaumu pia usikate tamaa mpaka ufikie malengo yako
Cha kushangaza wanafunzi wasiojitambua huwa hawataki msaada wa kuwatoa katika utumwa wa kutojitambua ndio maana huwa wakali wa kutokubaliana na anayetaka kuwasaidia ,huku wengi wakibeza na kuweka mbele aidha pesa, uzuri, makundi na kujifanya wanafahamu mambo yote wanayoelekezwa Hivyo ni vyema mwanafunzi akibahatika kujigundua kuwa ana dalili za kutojitambua yambidi kujitafakari na kuanza kufuata utaratibu ili arudi kwenye mstari.kwa kufanya hivyo wana funzi wengi watafaulu mitihani yao
jambo la pili
mwanafunzi anatakiwa kufuata na kutii maelekezo yote anayopewa na walimu, wazazi, na jamii inayomzunguka.pia kujifunze kuchuja baadhi ya mabo ili kuweze kufikia malengo, na siku zote mtu mwenye kutii hufanikiwa katika mipango yake.
acha kabisa tabia ya kuwa na makundi hatarishi ambayo yatakupotezea mda wako, na kukufanya ujiingize katika mambo yaliyo kinyume na maadili na badala yake jijengee tabia ya kujisomea katika makundi lakini pia jiwekee mda wa kusoma pekeyako katika sehemu tulivu.Uliza maswali ili kupanua ufahamu wako na kuweka kumbukumbu ya kile unachofundishwa ama kuelekezwa. Pia kuwa ni mwenye kuhitaji kujifuza {mdadisi}kila kukicha hakikisha umejifunza kitu kipya katika masomo yako.
jambo la tatu
waalimu wanapaswa kuwa na maelewano mazuri na wanafunzi lakini pia mkuu wa shule ahakikishe anawafuatilia waalimu wake kuona kama kweli mwalimu wa somo husika anaeleweka katika ufundishaji wake? na je vipimo vya mitihani inayotolewa wanafunzi wanafaulu katika viwango stahiki?.mkuu wa shule anatakiwa kutofumbia macho walimu wazembe na walimu wasiyoweza kuwaelekeza vema wanafunzi katika ufundishaji wao
mwisho
walimu wawajengee wanafunzi mazingira ya kujisomea kama vile kuwajengea utamaduni wa kukaa kimya wawapo madalasani, majadiliano kwa vikundi, mitihani ya kila wiki,morning speech, bila kusahau home
work.mfanye mwanafunzi apende na afurahie kusoma.
pia kua na mawasiliano mazuri baina yawazazi wa wanafunzi na walimu {mkuu wa shule}jenga mazoea ya kutoa taarifa ya maendeleo ya mwanafunzi kwa mzazi wake ili kuweza kumsaidia mwanafunzi katika masomo yake.
KARIBU MCHUNGUZI OPEN SCHOOL KWA ELIMU BORA. UKIWA MCHUNGUZI KUFAULU NI LAZIMA!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni