welcome

welcome

Jumatano, 16 Machi 2016

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA UFAULU WA MWANAFUNZI

kwanza

       mwanafunzi anatakiwa ajitambue kwamba yeye ni nani, na wajibu wake ninini kama mwanafunzi na kuachana kabisa na mambo ya kufuata mikumbo isiyo faa.Ninapozungumzia kujitambua ninamaanisha kuwa   uelewa wa mtu binafsi katika kungamua yeye ni nani,anapaswa kufanya nini, kwa sababu ipi.lini na katka muktadha upi.
          Elimu hii ya kujitambua ni adimu mno! Kwani hujikita ndani ya nafsi ya mtu na kumfanya kuonekana mwenye busara na hekima katika uongeaji ,kimaamuzi na kimatendo.

faida kuu za kujitambua

-Kila akifanyacho mwanafunzi anayejitambua hulenga kuchochea na kuleta maendeleo katika masomo yake
Ø Kuwa na msimamo dhabiti katika masomo bila kuyumbishwa na mtu yoyote.
Ø Kufikia malengo chanya.
Ø Huwa kioo cha jamii (unakuwa barua isomwayo na kila mtu katika jamii).
Ø Kutenda matendo mema ikiwemo nidhamu uwapo ndani ya shule,na katika jamii inayokuzunguka

Ø Kuwa mtu usiyekuwa na makuu, pia kuwa na matumizi mazuri ya rasliamali.mfano raslimali watu,,pesa n.k 
Ø uwe ni mtu wa watu.
Ø uwe mbunifu (Creative) husoma nyakati.
Ø Toa suruhu katika jambo linalokusibu na sio kulalamika au kuanza kulaumu pia usikate tamaa mpaka ufikie malengo yako
Cha kushangaza wanafunzi wasiojitambua huwa hawataki msaada wa kuwatoa katika utumwa wa kutojitambua ndio maana huwa wakali wa kutokubaliana na anayetaka kuwasaidia ,huku wengi wakibeza na kuweka mbele aidha pesa, uzuri, makundi na kujifanya wanafahamu mambo yote wanayoelekezwa Hivyo ni vyema mwanafunzi akibahatika kujigundua kuwa ana dalili za kutojitambua yambidi kujitafakari na kuanza kufuata utaratibu  ili arudi kwenye mstari.kwa kufanya hivyo wana funzi wengi watafaulu mitihani yao

jambo la pili

mwanafunzi anatakiwa kufuata na kutii maelekezo yote anayopewa na walimu, wazazi, na jamii inayomzunguka.pia kujifunze kuchuja baadhi ya mabo ili kuweze kufikia malengo, na siku zote mtu mwenye kutii hufanikiwa katika mipango yake.

acha kabisa tabia ya kuwa na makundi hatarishi ambayo yatakupotezea mda wako, na kukufanya ujiingize katika mambo yaliyo kinyume na maadili na badala yake jijengee tabia ya kujisomea katika makundi lakini pia jiwekee mda wa kusoma pekeyako katika sehemu  tulivu.Uliza maswali ili kupanua ufahamu wako na kuweka kumbukumbu ya kile unachofundishwa ama kuelekezwa. Pia kuwa ni mwenye kuhitaji kujifuza {mdadisi}kila kukicha hakikisha umejifunza kitu kipya katika masomo yako.

jambo la tatu 

waalimu wanapaswa kuwa na maelewano mazuri na wanafunzi lakini pia mkuu wa shule ahakikishe anawafuatilia waalimu wake kuona kama kweli mwalimu wa somo husika anaeleweka katika ufundishaji wake? na je vipimo vya mitihani inayotolewa wanafunzi wanafaulu katika viwango stahiki?.mkuu wa shule anatakiwa kutofumbia macho walimu wazembe na walimu wasiyoweza kuwaelekeza vema wanafunzi katika ufundishaji wao

mwisho

walimu wawajengee wanafunzi mazingira ya kujisomea kama vile kuwajengea utamaduni wa kukaa kimya wawapo madalasani, majadiliano kwa vikundi, mitihani ya kila wiki,morning speech, bila kusahau home 
work.mfanye mwanafunzi apende na afurahie kusoma.
pia kua na mawasiliano mazuri baina yawazazi wa wanafunzi na walimu {mkuu wa shule}jenga mazoea ya kutoa taarifa ya maendeleo ya mwanafunzi kwa mzazi wake ili kuweza kumsaidia mwanafunzi katika masomo yake.

KARIBU MCHUNGUZI OPEN SCHOOL KWA ELIMU BORA. UKIWA MCHUNGUZI KUFAULU NI LAZIMA!! 

Swahili - Soma

Jumanne, 16 Februari 2016

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2015



 
Baraza la Mitihani la Tanzania limekuwa likipigiwa simu na watu mbalimbali wakiomba ufafanuzi kuhusu taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imetangaza kuwa matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2015 yamezuiwa kwa muda hadi tarehe 08/03/2016. 

Magufuli Ataka Bandari Zilindwe Na Jeshi La Polisi Kama Ilivyokuwa Hapo Awali




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelitaka jeshi la polisi nchini kurejesha kitengo cha ulinzi bandarini na pia eneo ambalo linafungwa mita za mafuta.

Jumatatu, 15 Februari 2016

BREAKING NEWSSS, FORM FOUR RESULT 2015 OUT


The form four result are out watch from the link below or official website.Girls performed very well than boys.